Viungo

Fatawa

Masuala

Dua

Tarehe

Sira

Fiqhi

Sunna

Qurani

Maskani

Habari

Elimu

Afya
Nchi
Michezo
Vyakula
Riyadha
Masomo
Nasiha
Kamusi
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
      

 

      SERA

 

MAISHA YA MTUME

 

       
       
       
       

 
17-
  Kosa ya warusha mishale
18-
  Kuuliwa kwa Ubay bin Khalaf
19-
 
Fatma amtibu baba yake
20-
 
Abu Sufyan ajinaki
21-  Waliokufa na waliojeruhiwa
22-
 
Kuzikwa kwa mashahidi
23-
 
Waislamu warudi Madina
24-
 
Shambulizi la Ghaba
25-
 
Shambulizi la Hamraal-Asad
26-
 
Mwaka wa nne
27-
 
Kikosi cha Abu Salama
28-
 
Tume ya Ar-Raji'i
30
-  Maafa ya Bir Mauna
31
-  Shambulizi dhidi ya Bani Nadhir
32-  Shambulizi la Najd
33-  Shambulizi la Badr la pili
 


1-      Shambulizi dhidi ya Bani Qaynuqaa
2-      Kutolewa nchi Bani Qaynuqaa
3-      Shambulizi la Suwaiq
4-      Sala ya mwanzo ya Idi
5-      Kuolewa kwa Fatma binti wa Mtume
6-      Kubadilishwa Qibla
7-      Kufaridhiwa Saumu ya Ramadhani
8-      Kufaridhiwa Zaka
9-      Mwaka wa tatu
10-    Shambulizi dhidi ya Ghattafan
11-    Kuuliwa Kaab bin Al Ashraf
12-
 
  Shambulizi la Buhrani
13-
 
  Kikosi cha Zayd bin Haritha
14-
 
  Shambulizi la Uhud
15-
 
  Abdullahi bin Ubay aasi
16-
 
  Mapambano yanaanza
 

 

Shambulizi dhidi ya Banu Qaynuqaa: 

          Ushindi mkubwa walioupata Waislamu katika vita vya Badr haukuzidisha isipokuwa chuki kwa Mayahudi, na wakawa wanakereka sana kuwaona Aus na Khazraj na Muhajirina wako kitu kimoja wameshikana na kupendana, na wakawa kila kukicha wanafanya vitimbi vyengine hapo Madina kuwaudhi na kuwakera Waislamu, wakisahau kama wamefanya mkataba wa sulhu na Mtume (SAW), na kwa kuwa wao walikuwa ni watu wa biashara, na Waislamu walikuwa wanaamiliana nao kwa mambomengi kama kukopa, na kuuza na kununua, basi walikuwa daima wanawadhikidhiki na kuwakandamiza, tangu walikuwa wakiwafanyia wanaume katika wao mpaka wakaanza kuwaingilia wanawake.

        Waislamu walisubiri maudhiko hayo kwa muda mkubwa, lakini yalipozidi maudhiko, Mtume (SAW) aliwaita na kuzungumza nao na kuwanasihi kuacha jeuri na dhulma na uadui, na kuwakumbusha mkataba wao na Waislamu, na kuwataka wasilimu na kuwahadharisha kuwa yanaweza kuwatokea kama yaliyowatokea Makureshi, lakini Mayahudi wa Banu Qaynuqaa  waliokuwa wakiishi sehemu moja ya Madina, walimjibu Mtume (SAW) na kumwambia: Usighurike na nafsi yako kuwa wewe umeweza kuwaua watu kidogo katika Makureshi. Wao walikuwa hawajui kupigana, lakini wewe ukija kupigana na sisi, utajua kuwa umekumbana na watu, na kuwa hujawahi kukutana na watu kama sisi. Mwenyezi Mungu akateremsha Wahyi na kuwaambia: Q.3:12-13. 

          Waislamu waliendelea kusubiri mpaka safari moja alipokwenda mwanamke mmoja wa kiislamu katika soko zao, akaingia duka la sonara, wakata lazima afungue uso wake, na alipokataa waliifunga kwa hila nguo yake kwa nyuma alipoinuka uchi wake ukaonekana. Hapo tena akasimama Muislamu aliposikia kelele za yule mwanamke na kumuua yule sonara, na Mayahudi wakamvamia na kumuua. Watu wa yule Muislamu wakapiga kelele kuwaita Waislamu wengine na hapo vikaanza vita vikubwa vilivyosababisha kutolewa nchi kabila la Banu Qaynuqaa na kuondoshwa mzizi wao wa fitna.

Kutolewa nchi Banu Qaynuqaa:

            Tukio hili la uchokozi wa Banu Qaynuqaa, na kuvunja kwao ahadi na mkataba baina yao na Waislamu, kulimfanya Mtume (SAW) asiweze kusubiri tena, na kwa hivyo akakusanya jeshi lake na kumpa bendera Hamza ami yake na kumweka Abu Lubaba bin AbdulMundhir kuwa ndiye mwakilishi wake Madina na kuwaendea Banu Qaynuqaa. Mayahudi hawa walipoona jeshi la Mtume (SAW), kama desturi yao, walikimbia na kujificha kwenye ngome zao na kubaki humo humo ndani. Mtume (SAW) alizuzunguka nyuma zao na kuwasubiri nje kwa muda wa siku kumi na tano mpaka ikawajaa khofu na kuona kuwa hawawezi kustahmili tena. Hapo walikubali kumwachia Mtume (SAW) mali zao zote ili awaachie waondoke kwa salama wao na wake zao na watoto wao, na Mtume (SAW) akakubali na akamwakilisha Ubada bin Samit kuwatoa mji, wakaondoka na kuelekea kijiji kimoja kinachoitwa Azriat kilichoko huko Sham na kukaa huko mpaka wengi wao wakafa

            Mtume (SAW) akachukuwa mali yao na kutoa khumsi (nusu moja katika tano) na kuwapa jamaa zake Banu AbdulMuttalib na Bani Hashim waliosimama naye tangu mwanzo, na kugawa sehemu zilizobaki kwa Waislamu wengine

Shambulizi la Suwaiq: 

            Wakati watu walipokuwa wanapigana vita vya Badr, Abu Sufyan alikuwa hayupo maana alikuwa anarudi na msafara wake kuelekea Makka. Jambo hili lilikuwa likimsumbua sana mpaka aweka nadhiri kuwa kichwa chake hakitagusa maji mpaka aende akamshambulie Muhammad kulipiza kisasi kwa kuuliwa mwanawe na jamaa zake. Na ili aondoshe nadhiri yake hii, alitoka na watu mia mbili na kuelekea Madina. Alipokaribia Madina alikutana na kabila la kiyahudi la Banu Nadhir na kujaribu kuwashawishi wawasaidie katika vita vyao dhidi ya Waislamu. Walipokubali, Abu Sufyan alipeleka baadhi ya Makureshi kwenda Madina na kuchoma baadhi ya mitende yake, na wakakutana na Ansari mmoja na kumuua. Mtume (SAW) aliposikia haya, alitoka na jeshi la watu mia mbili, akimwakilisha juu ya Madina Bashir bin AbdulMundhir na kuwafuatia, lakini wao walikimbia sana mpaka wakawa wanatupa suwaiq njiani ili wazidi kuwa wepesi, na kwa hivyo Waislamu hawakuweza kuwafikia.

Sala ya mwanzo ya Idi: 

            Mwaka huu ndio mwaka wa kwanza ambao Mtume (SAW) aliwakusanya Waislamu akasali nao Sala ya Idi, na Sunna hii tukufu ni yenye faida kubwa kwa Waislamu, kwani Sala za Idi hukutanisha watu na kuwafanya watu wasaidiane katika siku za sherehe kama hizi, kwa kutoa Zaka za Fitri kwenye Idil-Fitri na kuchinja na kugawa nyama siku za Idil-Adh-ha zikawasaidia maskini, na kwa hivyo Waislamu wote kwa jumla wanakuwa katika furaha.

Kuolewa kwa Fatma binti wa Mtume (SAW). 

            Aidha, katika mwaka huu wa pili, aliolewa Fatma binti wa Mtume (SAW) akiwa ni mwenye umri wa miaka kumi na tano na Ali bin Abi Talib akiwa ni mwenye umri wa miaka wa miaka ishirini na moja, na katika mwaka huu vile vile Aisha aliingia nyumbani kwa Mtume (SAW) akiwa ni mwenye umri wa miaka tisa.

Kubadilishwa Qibla

            Katika mwezi wa Shaabani wa mwaka huu wa pili, Mwenyezi Mungu alimwaamrisha Mtume wake (SAW) kugeuza uso wake na kuelekea Qibla ambacho alichokuwa akitamani na kupendelea aelekee. Mtume (SAW) tangu alipohamia Madina alikaa zaidi ya mwaka na miezi minne anaelekea Jerusalemu kwenye Baytil-Maqdis, lakini hamu yake yote ilikuwa ni kuelekea Makka kwenye msikiti mtukufu uliojengwa na Nabii Ibrahim na Nabii Ismail, mpaka Mwenyezi Mungu akamtakabalia dua yake na kumuamrisha aelekee Makka, na wakati ulipokuja Wahyi wa kumuamrisha jambo hili alikuwa yeye na Waislamu ndani ya Sala, basi akageuka hapo hapo na Waislamu nyuma yake wakamfuata. Tukio hili liliwafanya Mayahudi kukasirika sana na kuwafanya wale waliokuwa wamejitia Uislamu katika wanafiki kutoka katika dini na kwa hivyo Uislamu ukasafika na watu wanafiki na wenye nyoyo dhaifu. Aidha, tukio hili likawafahamisha Waislamu kuwa Mwenyezi Mungu ni zake sehemu zote za ulimwengu zikiwa ni Mashariki au Magharibi.

Kufaridhiwa Saumu ya Ramadhani: 

            Aidha, katika mwezi huu wa Shaabani, Mwenyezi Mungu akawafaridhishia Waislamu Saumu ya Ramadhani na kuwa ni nguzo mojawapo kubwa katika nguzo tano za Uislamu ambazo Uislamu unazitegemea katika kunadhimisha maisha ya Waislamu, kwani katika kufunga saumu kunawafundisha Waislamu taabu na shida wanazozikuta maskini na mafakiri katika maisha yao ya uhitaji na njaa na namna gani wanahisi wakiwa katika hali hii. Halikadhalika, wakafaridhiwa Waislamu Zaka ya Fitri baada ya kumaliza Saumu zao ili ndugu zao wakiislamu wasipate taabu na shida siku za Idi na waweze kusherehekea sikukuu hii tukufu kama wenziwao wengine. Kabla ya kufaridhiwa Saumu hii ya Ramadhani, Mtume (SAW) alikuwa akifunga siku tatu za kila mwezi wa kiislamu

Kufaridhiwa Zaka:

             Vile vile, Mwenyezi Mungu aliwafaridhia Waislamu katika mwaka huu, Zaka ya mali zao kwa wale miongoni mwao wenye mali nyingi, na kuwahimiza watoe kutokana na mali zao zikiwa ni dhahabu au fedha, au mifugo na mazao, au biashara na mali nyenginezo fungu fulani kuwapa ndugu zao maskini, na kwa hivyo Uislamu ukaweka nidhamu ya kuchukuwa mali kutokana na matajiri na kuwapa ndugu zao mafakiri ili kuwasaidia na wao waishi maisha mazuri. Mwenyezi Mungu akawaambia kuwa: Q.Tauba:60.

Mwaka wa tatu:

Shambulizi dhidi ya Ghattafan:

            Mwanzo mwanzo wa mwaka wa tatu, katika mwezi wa Muharram (mfungo nne), Mtume (SAW) alipata habari kuwa kabila la Bani Thaalaba limejikusanya kutaka kuishambulia Madina. Mtume (SAW) akamweka Uthman bin Affan Madina kama mwakilishi wake, naye akatoka na jeshi la watu mia nne na khamsini na kuwapandia majabalini. Waliposikia kuwa wanajiwa, walikimbia na kutawanyika, lakini mmoja wao alikamatwa na baada ya kuzungumza na Mtume (SAW) alikubali kusilimu na akawa ni dalili wao wa kuwaonyesha njia kuliendea kabila lao na Mtume (SAW) aliendelea kuwafuata mpaka akafika sehemu ambayo walikuwa wamejikusanya kwenye maji yanayoitwa Dhi-Amar, na kukaa hapo kwa muda wa mwezi mzima kuwaonyesha hao Bani Thaalaba na Waarabu wengine nguvu za Waislamu na kuwatishia wasijaribu kutaka kuihujumu Madina, kisha baadaye akarudi Madina.

Kuuliwa Kaab bin Al-Ashraf:

            Kaab bin Al-Ashraf alikuwa ni mshairi mzuri wa kabila la Tai, na mamake alikuwa ni Myahudi wa kabila la Bani Nadhir, na alikuwa ni mtu tajiri na mwenye sura nzuri katika Waarabu, lakini alikuwa ni mwenye kumuudhi sana Mtume (SAW) kwa mashairi yake. Walipouliwa watukufu wa kikureshi katika vita vya Badr, alisikitika sana na kumtukana sana Mtume (SAW) na kuwatusi wanawake wa Masahaba, basi Mtume (SAW) likamuudhi sana hilo na kuwauliza Masahaba: Nani atatumalizia Kaab bin Al-Ashraf? Kwani yeye amemuudhi Mwenyezi Mungu na Mtumewe. Akasimama Muhammad bin Maslama na kusema: Mimi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unataka nimuue? Mtume (SAW) akasema: Naam.

            Basi akatoka Muhammad bin Maslama na Abu Naila na kwenda mpaka kwenye ngome ya Kaab, na Abu Naila ambaye alikuwa amenyonya naye alimpigia kelele akateremka, kisha wakamkamata na kumuua, kisha wakarudi kwa Mtume (SAW) na kupiga takbiri, akajua kuwa wamefaulu kwa lile waliloliendea, na alipoona kichwa chake mbele yake, alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumuondoshea udhia wa dhalimu huyu. Mayahudi waliposikia kuwa jabari lao limeuliwa waliingiwa na khofu kubwa na kihoro kuwamiliki nyoyo zao, na wakajua kuwa Mtume (SAW) hana mchezo, wakati wowote atataka kutumia nguvu hapana litakalomzuiya, basi wakaogopa na kunyamaza kimya, wasifanye lolote kwa mauaji ya dhalimu huyu.

Shambulizi la Buhrani:

            Katika mwaka huu wa tatu vile vile, Mtume (SAW) alipata habari kuwa watu katika kabila la Bani Suleym wanataka kuishambulia Madina, basi akamweka Madina Ibn Umm Maktum kama mwakilishi wake, na kutoka na jeshi la watu mia tatu kuwaendea, na walipofika mji uitwao Buhrani sehemu za Hijazi aliwakuta wametawanyika, na kwa hivyo hakukutokea vita vyovyote, basi akarudi Madina baada ya kukaa hapo muda mdogo.

Kikosi cha Zayd bin Haritha: 

            Baada ya vita vya Badr, mambo yaliwaharibikia sana Makureshi, maana njia yao ya kwenda Sham ambayo ilikuwa inapitia Madina ilikuwa imefungwa, na wanaogopa kuipita kwa kuchelea kuchukuliwa mali yao, na bila ya biashara mambo hayendi, basi wakapewa shauri na Al-Aswad bin AbdulMuttalib la kupitia njia ndefu ya mzunguko inayopita Iraq kwendea Sham, na wao wakaona rai nzuri, na akatoka Safwan bin Umayya akiongoza msafara kuipitia hii njia mpya. Habari za msafara huu zikamfikia Mtume (SAW) naye akamtoa Zayd bin Haritha na kikosi cha watu mia kuwachunguza, na walipofika Najd, waliuona msafara na kuuvamia, na Makureshi wakatoka mbio na kukimbizana. Mtume (SAW) akachukuwa ghanima hii na kuigawa kama desturi yake.

Rudi Juu

Shambulizi la Uhud

            Juu ya hasara walizozipata Makureshi katika vita vya Badr kwa kuuliwa watukufu wao, na hasara za mali katika mashambulizi mbali mbali, lakini wao waliendelea na inda na inadi zao na kushikilia kutaka kuwamaliza Waislamu kwa kila njia. Kwa hivyo, wakakubaliana Makureshi kuwa lazima viwepo vita vikubwa baina yao na Waislamu ili walipize kisasi na wawamalize Waislamu moja kwa moja.

            Katika waliokuwa na moto sana na jambo hili, na walioingiwa na mori kutaka lazima vita visimame na kuvipalilia, ni Ikrima mtoto wa Abu Jahl, na Abu Sufyan bin Harb, na Safwan bin Umayya, na Abdullahi bin Abi Rabia, wakawa daima wanawachochea Makureshi na kuwatia hamasa wapigane na Waislamu. Basi wakaanza kukusanya mali ya kuliunda jeshi na kulizatiti sawasawa, wakakusanyika kiasi cha Makureshi elfu tatu na wenziwao wa makabila mengine na kutumia baadhi ya washairi kuvutia Waarabu wengine kujiunga na jeshi hili.

            Aidha, akatoka Jubeyr bin Mutt'im na kumshawishi kijana wa kihabushia ambaye alikuwa ni mtumwa na jina lake akiitwa Wahshiy na alikuwa ni mtu mwenye shabaha sana hakosi akitupa mkuki wake, na kumwambia kuwa wewe ukiweza kumuua Hamza, ami yake Muhammad, basi utakuwa huru. Kisha likasimama jeshi likifuatwa na waimbaji wa kike na ngoma na mazumari na ulevi na watukufu wao wakachukuwa wake zao na watoto wao kushuhudia vita na kuwazidisha hamasa wasirudi nyuma vikishtadi vita.

            Mtume (SAW) akaletewa habari na ami yake Al-Abbas bin AbdulMuttalib kuwa jamaa wanakuja huko na wamedhamiria shari, basi Mtume (SAW) akawaita Masahaba na kuwauliza kama wabakie ndani ya mji kuwasubiri waingie au wawatokee. Wakubwa wa Masahaba wakatoa rai ya kubakia mjini, lakini vijana pamoja na Hamza wakasema bora tuwafuate nje. Basi Mtume (SAW) akavaa nguo zake za kivita na kuchukuwa ngao na upanga wake na kusimama kwa vita. Baadhi ya Maansari wakawaambia vijana kuwa si sawa walivyofanya na ilikuwa uzuri wachukuwe rai ya Mtume (SAW), lakini walipomuuliza, akawaambia: Haiwi kwa Nabii kuvaa silaha yake kisha akaivua mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu baina yake na maadui zake.

            Kisha Mtume (SAW) akaligawa jeshi vikosi vitatu: Muhajirina kikosi kimoja, na Maansari vikosi viwili, kikosi cha Aus na kikosi cha Khazraj. Akampa bendera ya kikosi cha Muhajirina Mus'ab bin Umeyr, na akampa bendera ya kikosi cha Aus, Usayd bin Khudhayr, na akampa bendera ya kikosi cha Khazraj, Hubab bin Al-Mundhir. Idadi ya vikosi vyote vitatu ilikuwa ni watu elfu moja, na akamweka Ibn Umm Maktum kuwa ni mwakilishi wake hapo Madina. Akatoka na jeshi lake mpaka alipopanda kilima aliona jeshi jengine akauliza ni nani hawa, akaambiwa hawa ni marafiki wa Abdullahi bin Ubay katika Mayahudi wanataka kusaidia kupigana na washirikina. Akasema: Je, wameshasilimu. Akaambiwa: La. Akasema: Sisi hatuwezi kuchukuwa msaada wa Makafiri dhidi ya Washirikina. Akaamuru warudi.

             Alipofika mahali panaitwa Sheikhan alisimama kukagua jeshi lake na kurudisha wale waliokuwa wadogo, na katika hao ni Raafi' bin Khadij na Samura bin Jundub, lakini akaambiwa Raafi' ni hodari wa kutupa mishale akamwacha, Samura akalia na kusema: Mimi nina nguvu zaidi kuliko Raafi' na ninamshinda kwa miereka. Basi Mtume (SAW) akawaamrisha wapigane miereka na Samura akamshinda Raafi' basi akamruhusu kubakia. Ulipoingia usiku wakasali Sala ya Maghribi, kisha ya Isha, na kuamua kulala hapo na akachagua watu khamsini kulinda kambi usiku, na kumweka Muhammad bin Maslama Al-Ansari kuwa ndio kiongozi wao, na Dhakwan bin Abd Qays kuwa mlinzi wa Mtume (SAW).

Abdullahi bin Ubay anaasi:

            Mkubwa huyu wa wanafiki, Abdullahi bin Ubay, alipoona kuwa ukweli ushadhihiri na hapana njia ya kuvikimbia vita baada ya kuwa vishawadia, aliondoka akichukuwa pamoja na yeye watu kiasi cha mia tatu, takriban thuluthi ya jeshi, na kudai kuwa Mtume hakumsikiliza rai yake ya kubakia Madina, na kwa hivyo hana haja ya kujiua nafsi zao kwa ajili yake. Akasimama Abdullahi bin Haram kumfuata na kujaribu kuwakinaisha wasimtupe Mtume wao, na kuwalaumu kwa kuondoka, lakini bila ya faida

            Baada ya uasi huu uliofanyika, Mtume (SAW) alitoka na watu mia saba na kuwaendea maadui mpaka akateremka kwenye njia mojawapo ya jabali la Uhud na kufunga kambi akiwa ameelekea Madina, na kulipa mgongo jabali la Uhud. Hapo Mtume (SAW) akalipanga jeshi lake, na kuchagua warusha mishale kiasi hamsini na kuwaamrisha wakae juu ya jabali chini ya uwongozi wa Abdullahi bin Jubayr Al-Ansari, na kuwaamrisha wasiondoke hapo walipo wakishinda wakishindwa. Kisha akazipanga safu za jeshi lililobakia, na akamweka upande wa kulia Al-Mundhir bin Amr, na kushoto Az-Zubayr bin Al-A'wwam akisaidiwa na Al-Miqdad bin Al-Aswad. Halafu akasimama kutoa hotuba kuwatia hamasa Waislamu na kuwapa moyo, na kuwahimiza wasubiri, na wasipigane mpaka awaamuru.

            Kwa upande mwengine, Washirikina walikuwa kwenye bonde wakilielekea jabali la Uhud, akiwa upande wa kulia Khalid bin Al-Walid, na upande wa kushoto Ikrima bin Abi Jahl, na aliyekuwa akiongoza jeshi la wanaokwenda kwa miguu Safwan bin Umayya, na kiongozi wa warusha mishale ni Abdullahi bin Rabi'a, na hawa wote walikuwa chini ya uwongozi wa Abu Sufyan bin Harb ambaye alikuwa katikati ya jeshi. Kisha Abu Sufyan akajaribu kuleta fitna na kutia chokochoko baina ya Waislamu, akapeleka mtu kwa Maansari na kuwaambia: Tuwachieni sisi na binamu zetu, nasi tutakuwacheni, na tutakuwa hatuna haja ya kupigana na nyinyi. Lakini Maansari hawakuhadaika na maneno haya na wakamjibu maneno makali na kuzidi kumtia mori

            Wanawake wa kikureshi kwa upande wao, wakiongozwa na Hind bint Utba, mke wa Abu Sufyan, walikuwa wakipiga kelele na kuimba na kupiga vigoma na kuwatia mori wanaume wao, na kupita baina ya safu zao, na kuwashajiisha na kuwatia hamasa.

Mapambano yanaanza:

            Ilipowadia saa ya mapambano, makundi mawili yakakaribiana, na akatoka mmoja katika washika bendera kutoka kabila la Bani Abduddaar upande wa Washirikina,  na kutaka mtu yeyote katika Waislamu atoke kupambana naye. Akajitokeza Ali bin Abi Talib na kupambana naye na kumwangusha kutoka kwenye ngamia wake na kumuua mara moja. Kisha akasimama Az-Zubeyr na kupambana na mwengine na kumuua, na akasimama Hamza na kumuua yule aliyekuwa akipambana naye, mpaka wakauliwa kumi katika washika bendera wa Bani Abduddaar.

            Makundi yakaingiana na vita vikashitadi, na Waislamu wakazidi hamasa walivyoona ushindi uko kwao, na kwa imani yao kubwa wakaweza kuwaua wengi katika Washirikina, na akawa Abu Dujana ambaye alipewa upanga na Mtume (SAW) na kuambiwa autumie kwa haki yake, na alipouliza nini haki yake, aliambiwa asiutumie kumuua Muislamu, na akimuona kafiri asimwache, basi akatoka Abu Dujana na kutoa kitambaa chake chekundu na kujifunga kichwani, mwenyewe akikiita kitambaa cha mauti, akikifunga hicho basi hana isipokuwa kuua. Akatoka huku akenda kwa maringo na kupigana kwa ushujaa mkubwa sana akaua watu wengi sana. Mtume (SAW) akasema: Mwenyezi Mungu anauchukia mwendo huu wa maringo isipokuwa kwenye hali kama hii, yaani ya vita

            Kwa upande mwengine, Hamza alipigana kwa ushujaa mkubwa sana na kuua Washirikina wengi mpaka akawa yumo ndani ya safu za Makafiri, na hapo ndipo alipopata nafasi yule mtumwa wa kihabushia Al-Wahshiy kumrushia mkuki na kumuua, naye alikuwa ameahidiwa akimuua Hamza ataachwa huru. Kisha akaja Hind mke wa Abu Sufyan na kumpasua tumbo lake na kutoa ini lake na kulitafuna na kulitupa. Aidha, Makureshi wengi walikuwa wakiikatakata miili ya mashahidi wa kiislamu kwa chuki kubwa waliokuwa nayo

            Mwenyezi Mungu aliwapa ushindi mkubwa Waislamu mwanzo wa vita hivi, mpaka wakawaendesha mbio Washirikina na wakawa hawajui wanafanya nini. Huku juu ya jabali, warusha mishale walipoona kuwa wenziwao wameshinda na kila mmoja anakimbilia ghanima, tamaa ya dunia ikawaingia wakataka kwenda wawahi na wao sehemu yao, na juu ya kuwa mkubwa wao aliwakataza, lakini hawakusikiliza, wakateremka kinyume na amri ya Mtume (SAW) aliyowapa mwanzo wa vita ya kutopabanduka mahali hapo wakishinda wakishindwa.

Kosa la Warusha mishale:

            Hili lilikuwa kosa kubwa kabisa la kuasi amri ya Mtume (SAW) na kiongozi wao, na Mwenyezi Mungu akawaonyesha kuwa amri ya Mtume wake ilikuwa imekusanya hekima kubwa kabisa ya kivita, maana pale pale baada ya kuteremka juu ya jabali, Khalid bin Al-Walid ambaye alikuwa wakati huu ni mshirikina katika jeshi la Makureshi, aliitumia fursa hii na kuwapandia yeye na kikosi chake wale warusha mishale kidogo waliobaki na kuwaua, kisha wakawateremkia Waislamu chini waliokuwa wameshughulika kukusanya ghanima na kuwavamia kwa ghafla, wakababaika na kufazaika, na kutojua nini kinatokea, na washirikina waliokuwa wakikimbizana huku na huko waliona yaliyotokea wakarudi mbio kuwazunguka na kuwapiga Waislamu mpaka matokeo ya vita yakabadilika na ushindi ukageuka kuwa hasara na mauti.

            Waislamu wakazungukwa na kukimbizwa mbio na kufuatwa na kuuliwa mpaka akabaki Mtume (SAW) pekee na Masahaba zake kidogo waliomzunguka. Washirikina wakajaribu sana kumfikia Mtume (SAW) ili wamuue, lakini Masahaba zake walipigana kwa ushujaa mkubwa sana na kumkinga kwa silaha zao na miili yao mpaka ikajaa miili yao alama na athari za mishale na mikuki na panga. Na katika waliokuwa wakimhami na kumlinda kwa ushujaa mkubwa kabisa ni Saad bi Abi Waqqas ambaye alikuwa hodari sana wa kurusha mishale na Talha bin Ubaydillah ambaye alipigana mpaka ukapigwa mkono wake na kukatwa vidole vyake. Mtume (SAW) akamsifu na kusema: Mwenye kutaka kumtazama shahidi anakwenda juu ya ardhi, basi naamtazame Talha bin Ubaydillah.

            Mtume mwenyewe (SAW) katika vita hivi yaliyomfika si madogo, kwani alitupiwa jiwe, na kupasuliwa mdomo, na kuumizwa kipaji na kutolewa damu nyingi, na katika hali hii mbaya, walisikia Masahaba wengine sauti ya Mtume wao akiwaita wakarudi mbio kuja kumlinda na wakamzunguka na kumhami kwa miili yao, na katika hao ni Abubakar Assiddiq, na Ali bin Abi Talib, na Umar bin Al-Khattab, na Mus'ab bin Umeyr, na AbdulRahman bin Awf na Abu Dujana, na Sahl bin Hanif, na Malik bin Sinan, na Qatada bin Nuuman, na Umm A'mmara Nusayba bint Kaab.

            Kila mmoja katika hawa walisimama kumhami Mtume (SAW) kwa ushujaa mkubwa na kupata majeruhi mengi kwa namna Washirikina walivyokuwa wanawajia makundi kwa makundi kuwahujumu, na katika wanawake waliopigana sana kumlinda Mtume ni Nusayba (Umm Ayman) ambaye alipigana mpaka akajeruhiwa sehemu kumi na mbili, na akapigana Mus'ab bin Umeyr mpaka akauliwa, na kwa kuwa alikuwa anafanana na Mtume (SAW), alidhani Ibn Qam-a kuwa amemuua Mtume akapiga kelele kutangaza kuwa amemuua Muhammad na pale pale habari ya kuuliwa Mtume (SAW) ikaenea kwa Washirikina na Waislamu wakavunjika moyo na kuanza kubabaika mpaka wakawa wanapigana wenyewe kwa wenyewe.

             Baada ya kuuliwa Mus'ab bin Umeyr, alichukuwa Mtume (SAW) bendera na kumpa Ali bin Abi, na kujaribu kuliendea jeshi lake, na hapo Kaab bin Malik akamuona na kumtambua na kujua kuwa Mtume bado hakufa. Akapiga ukelele mkubwa kuwabashiria Waislamu kuwa Mtume yu hai. Pale pale Waislamu wakaja kiasi cha Masahaba thalathini na kumzunguka. Washirikina ambao vile vile walisikia kuwa Mtume (SAW) hakufa walimfuatia kutaka kumuua, lakini Waislamu waliokuwa wakipigana kwa ushujaa na kumhami Mtume wao kwa nguvu zao zote, hawakuwapa fursa hata chembe, na Mtume (SAW) akapata nafasi ya kurudi nyuma na kuingia kwenye njia katika jabali. Kisha Mtume (SAW) alitaka kupanda juu ya jabali, lakini akashindwa, akaja Talha bin Ubaydillahi na kumbeba mpaka akalipanda

Kuuliwa kwa Ubay bin Khalaf:

            Baada ya kutulia katika jabali alikuja Ubay bin Khalaf na kutaka kumuua Mtume (SAW). Mtume akawaambia Masahaba wamuache, basi alipokaribia alichukuwa Mtume (SAW) mkuki na kumkabili, kisha akamrushia na ukamwingia kidogo kwani alikuwa amevaa nguo za kinga, lakini sehemu ndogo iliyomuingia ilisababisha mauti yake wakati walipokuwa wanarudi Makka. Na huyu ndiye mtu pekee ambaye Mtume (SAW) amemuua katika vita vyote alivyopigana.

            Washirikina wengine katika Makureshi wakiongozwa na Abu Sufyan na Khalid bin Al-Walid walijaribu kupanda jabali ili wamfikie Mtume (SAW) na kumuua, lakini Umar bin Al-Khattab na kundi la Muhajirina lilisimama thabiti kumhami Mtume wao, wakapigana nao mpaka wakawaangusha kutokana na jabali. Saad bin Abi Waqqaas, kwa upande wake, aliwarushia mishale akiwaua mpaka wakakimbia, na hili lilikuwa hujuma la mwisho la Washirikina, kwani baada ya hapa walirudi nyuma na kuanza kuondoka kurudi Makka

Fatma amtibu babake:

            Mtume (SAW) alipofika kwenye jukwaa lake alilotengenezewa, alikuja Ali bin Abi Talib na kwenda kumletea maji, kisha akawa anammiminia kichwani na Fatma anampangusa uso na kumpangusa damu iliyokuwa ikimwagika. Kisha akachukuwa kipande cha jamvi na kukiunguza na kumwekea juu ya jeraha lake na kuzuiya damu isitoke. Kisha akaja Muhammad bin Maslama na kumletea maji mengine mazuri na kumpa anywe, akanywa na kumuombea kheri. Kisha akasali kwa kukaa kwa sababu ya udhoofu aliyokuwa nao kwa damu nyingi kumwagika, na Waislamu wakasali nyuma yake.

Rudi Juu

Abu Sufyan ajinaki

            Washirikina walipojikusanya na kuwa tayari kuondoka, alipanda Abu Sufyan jabali na kuwapigia Waislamu kelele: Je, yuko Muhammad kati yenu? Wasimjibu kitu. Akauliza: Yuko Ibn Abi Quhafa (Abubakar)? Asijibiwe kitu. Akauliza: Yuko Umar bin Al-Khattab? Asijibiwe kitu, maana Mtume (SAW) aliwakataza kumjibu. Lakini Umar alipoona anaendelea kujinaki, hakuweza kustahmili akamjibu na kumwambia kuwa wote hao uliowataja wa hai, ewe adui wa Mwenyezi Mungu. Abu Sufyan akataka kumuona Umar, na Mtume (SAW) akamwambia ajitokeze na akenda mpaka karibu yake. Abu Sufyan akamuuliza kama tumemuua Muhammad? Umar akamwambia: La, bali yeye hivi sasa anasikia maneno yako haya. Basi Abu Sufyan akamwambia Umar: Wewe ni msema kweli zaidi kwangu kuliko Ibn Qam'a na ni mwema zaidi. (Ibn Qam'a ndiye aliyeeneza habari ya kuuliwa Mtume (SAW). 

            Abu Sufyan akaondoka na Washirikina wenzake huku akinadi: Mwakani mkutano wetu Badr! Na Mtume (SAW) akamwambia mmoja katika Masahaba amjibu: Mwambie: Naam. Ni miadi baina yetu. Kisha akamtuma Ali bin Abi Talib kuwafuata Washirikina na kuwatazama nini wanapanda. Ikiwa watapanda ngamia basi wanaelekea Makka, na ikiwa watapanda farasi, basi wanaelekea Madina, na akaapa ikiwa wanaelekea Madina, basi atawafuata, na kupigana nao. Ali akawafuata na kuwakuta wamepanda ngamia akajua kuwa wanaelekea Makka.

Waliokufa na waliojeruhiwa:

            Baada ya kuondoka Makureshi, Waislamu walianza kuwapitia wenziwao waliopigana vita, na kutazama waliouliwa na waliojeruhiwa. Wakapatikana waliokufa ni kiasi watu sabiini, sitini na tano katika hao ni Maansari, wanne ni Muhajirina na mmoja ni Yahudi. Mtu huyu ambaye alikuwa ni katika Mayahudi wa Bani Thaalaba, aliwaambia watu wake kuwa mnajua kuwa kumnusuru Muhammad ni haki juu yenu, na wao wakamjibu kuwa leo ni siku ya Jumamosi, yaani ni siku wasiofanya kazi, basi yeye akatoka pamoja na Waislamu na kwenda kupigana na Washirikina mpaka akauliwa. Mtume (SAW) akasema: Mukhayriq ni Yahudi bora

            Aidha, katika waliojeruhiwa kwenye vita hivi, mtu mmoja anaitwa Usayrim (Amr bin Thabit). Waislamu walipomuona walistaajabu maana alikuwa hataki kusilimu, na walipomuuliza, alisema kuwa amekuja kupigana kwa ajili ya Uislamu, si kwa ajili ya watu wake, basi alipokufa walimtajia hili Mtume (SAW) naye akawaambia kuwa: Huyo ni katika watu wa Peponi. Naye kama anavyoeleza Abu Hureyra hakuwahi kusali hata mara moja. Na kwa upande mwengine, kuna mwengine katika waliojeruhiwa akiitwa Qazmaan, na huyu alipigana vita vikali na akauwa Makafiri wengi, lakini alifanya hivi kwa ajili ya watu wake na kabila lake, basi alipokufa Mtume (SAW) akasema kuwa huyo ni katika watu wa Motoni

Kuzikwa kwa Mashahidi: 

            Baada ya kuangalia Mtume (SAW) na Masahaba zake wale waliouliwa katika Waislamu na wale waliojeruhiwa, aliamrisha mashahidi wote wasioshwe, lakini watolewe nguo za chuma walizovaa na ngozi na wawachwe na nguo zao za damu na wazikwe hivyo hivyo, kwani Mwenyezi Mungu atawafufua siku ya Kiyama yakiwa majeraha yao yanatoa damu ikinukia miski, na wakawa wanafukiwa wawili wawili, na watatu watatu kwenye kaburi moja, na akakataza Mtume (SAW) kuhamishwa maiti na kupelekwa Madina, na akaamrisha wazikwe pale mahali walipofariki

            Kisha Mtume (SAW) akamuona ami yake Hamza na namna gani Washirikina walivyokatakata na kumpasua matumbo, na hili likamhuzunisha sana kufika hadi kulia sana, na alipokuja shangazi lake Safia anataka kumtazama nduguye alijaribu kumzuiya ili asione yale aliyofanyiwa, lakini Safia alishikilia na kusema kuwa yeye anajua nini alilofanyiwa na maadamu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi yeye yuko radhi na atasubiri, na baada ya kumtazama na kumuombea Mungu, aliamrisha Mtume (SAW) azikwe pamoja na Abdullahi bin Jahsh, na alikuwa ni mtoto wa dadake, na nduguye wa kunyonya

Waislamu warudi Madina: 

            Baada ya kuzikwa mashahidi, na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumnusuru, alishika njia kurudi Madina pamoja na Masahaba zake, na njiani akakutana na mwanamke ambaye mumewe, na kakake, na babake wamejeruhiwa katika vita, na walipomwambia aliuliza habari ya Mtume (SAW) akaambiwa kuwa hana neno, akataka aonyeshwe ili amuone mwenyewe, na baada ya kuonyeshwa alisema: Misiba yote baada yako ni midogo, kuonyesha mapenzi makubwa waliokuwa nayo kwa Mtume wao.

            Usiku wake akawasili Madina na alipofika kwa wakeze alimpa upanga wake bintiye Fatma na kumwambia aioshe damu iliyokuwa juu yake, na kadhalika Ali bin Abi Talib akampa mkewe Fatma upanga wake auoshe, na kumwambia kuwa upanga huu leo umefanya kazi. Mtume (SAW) akamwambia: Ikiwa umepigana kweli kweli leo, basi amepigana vile vile kweli kweli, Sahl bin Hanif na Abu Dujana.

            Waislamu wakaendelea kuwa na wasiwasi kuwa pengine Washirikina watarudi waihujumu Madina, wakawa wamacho wanalinda mji na kumlinda Mtume wao. Halikadhalika, Mtume (SAW) alikuwa ana wasiwasi na shaka kuwa Makureshi watarudi maana wameondoka lakini hakuna faida yoyote iliyopatikana, na ijapokuwa Waislamu wamepata hasara nyingi sana kwa kuuliwa watu wao, lakini Makafiri hawakuweza kumuua Mtume (SAW), wala kuuondosha Uislamu, wala kuchukuwa mali ya Waislamu baada ya vita. Basi asubuhi yake akawataka wale waliopigana vita watoke naye tena kuwafuata Makafiri na kupigana nao tena, kabla hawajafikiria kurudi na kuja kuiteka Madina

            Na kama alivyokuwa Mtume (SAW) anafikiria fikra hizi, Makureshi vile vile iliwapitikia fikra hii walipofika mji uitwao Ar-Rawhaa, wakazungumza na kulaumiana kuwa hapana faida iliyopatikana katika vita hivi, na kuwa bora warudi Madina na wawamalize.

Shambulizi la Ghaba: 

            Kabla ya shambulizi la Khaybar kwa siku tatu, kulitokea tukio ambalo lilisabibisha Mtume (SAW) kutoka na jeshi kwenda kumshambulia Uyayna bin Hisn na watu wake, na sababu yake ni kuwa Mtume (SAW) alikuwa na ngamia mwituni wanalishia, akaja AbdulRahman bin Uyayna na watu wake na kuvamia ngamia hawa na kumuua mchungaji wake

            Salama bin Al-Akwa'a alikuwa akitembea mwituni yeye na Rabah, akamuona AbdulRahman bin Uyayna amekuja na kuvamia ngamia na kuwakusanya na kuondoka nao. Ibnul-Akwa'a akamtuma Rabah kwenda Madina kumfikishia Mtume (SAW) habari hii, na yeye akapanda juu ya kilima na kupiga kelele kwa nguvu zake zote kuwazindua watu wa Madina. Kisha akakimbia mbio kuwafuata nyuma na kuwarushia mishale, wakawa wakitaka kumfuatia hukimbia mbio wasimpate, maana yeye alikuwa ni mkimbiaji mzuri sana wa kiansari, na wakigeuza farasi kwenda zao, huwafuata na kuwarushia mishale, mpaka wakawa ngamia wote waliowachukua wamebakia nyuma, na yeye yuko nao hawawachi

            Huku nyuma, Mtume (SAW) akatoka na jeshi la Masahaba zake na kumpa bendera Miqdad bin A'mr na kumwacha Ibn Umm Maktum kuwa mwakilishi wake hapo Madina, na kuelekea msituni mpaka akamfikia Ibnul-Akwa'a. Vikasimama vita baina ya jeshi la Mtume (SAW) na watu wa Uyayna. Al-Akhram akamkata miguu ya farasi wa AbdulRahman, na AbdulRahman akamchoma upanga Al-Akhram na kumuua. Kisha akamrukia farasi wa Al-Akhram na kumpanda. Abu Qatada akamfuatia AbdulRahman na kumchoma upanga, lakini akawahi na yeye kumkata miguu ya farasi wa Abu Qatada. AbdulRahman akaanguka na kufa, na Abu Qatada akamrukia farasi wa Al-Akhram aliyekuwa amempanda AbdulRahman na hapo waliobakia wakakimbia. Wakafa katika vita hivi Washirikina wawili na Muislamu mmoja.

            Waislamu wakarudisha aghlabu ya wanyama wao. Ibnul-Akwa'a akamwomba Mtume (SAW) ampe watu awafuate hawa waliokimbia, lakini Mtume (SAW) akamwambia: Umemiliki basi samehe. Kisha Mtume (SAW) akasema: Mbora wa wapanda farasi wetu leo ni Abu Qatada, na mbora wa watu wetu leo ni Salama, na akampakia nyuma wa farasi wake na kurudi naye Madina na kumpa sehemu mbili za ghanima.

Shambulizi la Hamraal-Asad:

            Baada ya kushauriana na Masahaba, Mtume (SAW) alimwakilisha Ibn Abi Maktum hapo Madina, na kumpa bendera Ali bin Abi Talib, na kutoka kuwafuatia Washirikina. Jeshi la kiislamu liliendelea na safari yake mpaka likafika Hamraal-Asad, mahali kiasi cha maili nane kutoka Madina akafunga kambi. Hapo akakutana na Maabad bin Abi Maabad akasilimu, naye akasikitika kwa yale yaliyomfika katika vita vya Uhud, na Mtume (SAW) akamtuma aende kwa Abu Sufyan na kumtishia.

            Alipofika Maabad kwa Abu Sufyan alimkuta kama vile alivyotarajia Mtume (SAW) kuwa keshajitayarisha na jeshi lake kurudi Madina kwenda kuwamaliza Waislamu, lakini alipomuona Maabad alimuuliza una nini? Na Maabad akamjibu na kumwambia kuwa Muhammad yuko njiani na amekusanya jeshi kubwa kuja kuwamaliza, basi yeye kwa kuwa hajui kama Maabad ameshasilimu, akamwambia kuwa na sisi tumejizatiti hivi tunataka kwenda kuwamaliza, basi akamnasihi asifanye hivyo, maana jeshi la Muhammad ni kubwa sana na kila mtu ana mori wa kutaka kuja kuchukuwa kisasi.

            Pale pale jeshi la Abu Sufyan likavunjika moyo na zikawatoka nguvu, na kuingiwa na khofu na kihoro, basi likaona bora waendelee na safari yao kurudi Makka, na ili Muhammad asiwafuatie na jeshi lake, alipata fursa ulipopita msafara wa Abd Qays unakwenda Madina, akawatuma na kuwaambia wamwambie Muhammad kuwa kuna watu njiani wamejikusanya kuja kuwapiga basi wajihadhari, na ulipopita msafara huu ukamkuta Mtume (SAW) na jeshi lake, ulimfikishia huu ujumbe, lakini Waislamu hawakuogopa, bali walizidi hamasa na imani.

            Mtume (SAW) aliendelea kukaa hapo Hamraal-Asad kwa masiku kidogo kabla ya kurudi Madina, lakini kabla ya kuondoka hapo alimkamata Abu Azza mshairi katika mateka wa Badr ambaye alimsamehe kwa umaskini wake na kuwa na watoto wengi wa kike wa kuwatazama, lakini baada ya kuachwa, hakusita kumtukana Mtume (SAW) na Waislamu kwa mashairi yake, basi akamuamrisha Az-Zubeyr amuue, maana Mtume (SAW) alimuambia: Muislamu hatafunwi katika shimo moja mara mbili, na kuwa walimwacha mara ya kwanza akarudia yale yale, basi Az-Zubeyr akamkata kichwa chake, na kuondosha fitna yake. Aidha, aliamuru auliwe Muawiya bin Mughira bin Abil-Aas ambaye alikuwa mmojawapo wa majasusi wa Makka

            Na kwa hakika shambulizi hili ni kama kiendelezo cha shambulizi la Uhud, maana baada ya kurudi Madina tu kutoka kwenye shambulizi la Uhud, Mtume (SAW) alikusanya jeshi lake na kuondoka siku ya pili yake kulifuata jeshi la Makka, na kuwaonyesha kuwa jeshi la Waislamu bado lina nguvu na liko tayari kupambana na maadui wa Mwenyezi Mungu. Matokeo ya vita vya Uhud kama tulivyoona ni mchanganyiko wa ushindi na hasara kwa pande zote mbili, mara ya kwanza walishinda Waislamu wakawatia hasara kubwa Washirikina na kuchukuwa mali yao, na mara ya pili ushindi ulikuwa ni wa Washirikina lakini hawakuweza kuukamilisha wala kupata ghanima zozote wala mateka yoyote, na kwa hivyo Mtume (SAW) aliona bora kuwafuata na kuwaonyesha kuwa Waislamu bado wana nguvu zao na hawakushindwa

Mambo muhimu yaliyotokea mwaka huu:

            Katika mwaka huu wa tatu vile vile, Uthman bin Affan alimuoa binti wa pili wa Mtume (SAW) Umm Kulthum baada ya kufa dadake Ruqayya ambaye ndiye aliyekuwa mkewe wa kwanza, na ndio maana akaitwa Uthman Dhun Nuurayn, yaani mwenye nuru mbili. Aidha, Mtume (SAW) alimuoa Hafsa binti wa Umar bin Al-Khattab, ambaye mumewe Khunays alikufa kwa majeraha aliyoyapata katika vita vya Badr, na vile vile Mtume (SAW) akamuoa Zaynab bint Khuzayma Al-Hilaliya ambaye alikuwa akijulikana tangu zama za Ujahili kwa jina la Ummul-Masakiin, yaani mama wa maskini, kwa ukarimu wake na kupenda kwake maskini, naye alikuwa kabla ameolewa na Abdullahi bin Jahsh kabla ya kuuliwa katika vita vya Uhud

            Aidha, katika mwaka huu uliharimishwa ulevi moja kwa moja, baada ya kunabihishwa Waislamu ubaya wake na uchafu wake, na wakaona Waislamu uovu wake kwa kutokea ugomvi baina ya Waislamu na uadui. Mwenyezi Mungu akateremsha Wahyi wake kuukataza moja kwa moja, na kusema: Q. Baqara:219; Nisaa:43; na Maida:91

            Waislamu wakauitika mwito huu wa Mwenyezi Mungu kwa hamasa kubwa na ulevi wote ukamwagwa na kusita kutumika, na hii ni kuonyesha imani kubwa waliokuwa nayo Masahaba na dini yao, na kumpenda kwao Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Rudi Juu

Mwaka wa Nne

            Mwaka huu ulijaa matokeo mbali mbali kwa sababu ya hasara waliyoipata Waislamu katika vita vya Uhud, kwani Makafiri na Washirikina walichukulia kuwa Waislamu wamekuwa dhaifu na kwa hivyo tunaweza kuwachezea tunavyotaka, na makabila mbali mbali yakaanza kupanga njama za kutaka kuhujumu Madina na kuwadhuru Waislamu. Aidha, Mayahudi nao kwa upande wao wakaingiwa na hamu ya kutaka kulipiza kisasi kwa yaliyowatokea wenziwao siku za nyuma, na wakawa wanapanga vitimbi hivi na hivi, na kudhihirisha uadui kwa Waislamu.

Kikosi cha Abu Salama: 

             Ili kuvivunja vitimbi hivi, Mtume (SAW) alikitayarisha kikosi mara tu aliposikia kuwa Banu Saad bin Khuzayma wanataka kuwapiga vita Waislamu, akampa bendera Abu Salama na kumpa kikosi cha watu mia moja na hamsini kwenda kuwapiga Banu Saad. Akatoka Abu Salama na kikosi chake cha Muhajirina na Maansari mwanzo wa mwezi wa Muharram na kwenda mpaka walipo Banu Saad na kuwahujumu, wakakimbizana bila ya kupigana nao, basi akarudi zake Madina na ghawira walizozipata za ngamia na mbuzi. Lakini Abu Salama hakuishi muda mkubwa baada ya hujuma hii, kwani majeraha aliyoyapata katika vita vya Uhud yalimpa taabu na kusababisha kifo chake.

            Katika mwezi huu huu, Mtume (SAW) anamtuma Abdullahi bin Uneys kwenda kwa Khalid bin Sufyan kuondosha fitina yake, kwani amepata habari kuwa anakusanya watu kutaka kuja kuwapiga vita Waislamu. Akamtoa peke yake ende kwake na adai kuwa anakuja kumsaidia. Basi alipofika kwake alizungumza naye na kumueleza kuwa amekuja kuwa naye akahadaika, na walipokuwa wamebaki peke yao, alimpiga upanga na kumkata kichwa na kurudi nacho kwa Mtume (SAW), mzizi wa fitina ukakatika

Tume ya Ar-Raji'i: 

            Katika mwezi wa Safar, walikuja watu kumuomba Mtume (SAW) awapelekee walimu ambao watawafundisha dini ndugu zao Waislamu katika kabila lao la A'dhal na Al-Qaara, na Mtume (SAW) akawapa walimu sita au kumi wakiongozwa na A'sim bin Thabit Al-Ansari, lakini walipofika njiani waliwageukia na kuwaashiria kabila la Huzeyl, kabila la yule Khalid bin Sufyan aliyepelekewa mtu akamuue, kuja kuwahujumu.

            Waislamu walipowaona walipanda juu ya jabali na kujaribu kuwakimbia, na wao wakawaambia kuwa teremkeni hatutakuueni, wakateremka watatu, na wengine wakakataa kuteremka basi wakapigana nao, na wao walikuwa ni watu zaidi ya mia, basi wakawaua. Wakabaki watatu na mmoja wao alipokataa kuwafuata, vile vile wakamuua, wakabaki wawili Khubayb bin A'diy na Zayd bin Ad-Dathana, wakawachukua mpaka Makka na kuwauza kwa wale ambao wana visasi nao vya tangu mauaji ya Badr, basi wakawaua.

Maafa ya Bir Mauna: 

            Katika mwezi huu huu wa Safar, yalitokea maafa mengine kwa Waislamu ukawa ni msiba mkubwa na kumsabishia Mtume (SAW) huzuni kubwa, kwani alikuja Abu Barraa A'amir bin Maalik Madina, na Mtume (SAW) akamueleza Uislamu naye hakuukataa wala hakuukubali, lakini alimwambia Mtume (SAW) kuwa jambo lako hili ninaliona ni zuri, kwa nini hupeleki watu wako Najd, wakawatangazia watu wa huko jambo hili, nami ninahisi watalikubali. Mtume (SAW) akamwambia: Mimi ninawaogopea watu wa Najd. Basi Abu Barraa akamwambia: Mimi nitawahami nao

            Mtume (SAW) akapeleka Masahaba kiasi ya hamsini au sabiini, wote wakiwa wamehifadhi Qurani uzuri, wakiongozwa na Al-Mundhir bin Amr ambaye alikuwa ni katika Waislamu wazuri, anayeujua Uislamu na kushikama nao na kuijua Qurani vizuri. Wakenda mpaka wakafika mahali panapoitwa Bir Mauna wakateremka na kufanya kambi, na kumpeleka Haram bin Milhaan na barua ya Mtume (SAW) kwa Aamir bin Tufeyl, alipofika na kumpa, hakuitazama wala hakuisoma bali alimuamrisha mtu amuue yule mjumbe, akaja na kumchoma mkuki, akafa huku akisema: Allahu Akbar, nimefuzu wallahi.

            Kisha Aamir bin Tufeyl akapeleka watu wake kutokana na makabila ya Bani Suleym (Ra'il na Dhakwaan na U'sayya) kwenda kuwaua waliobaki, na Abu Barraa alipowaambia kuwa hawa wako katika himaya yangu, hawakumsikiliza, bali waliwazunguka na kupigana nao mpaka wakawaua wote, isipokuwa Kaab bin Zayd bin An-Najjaar ambaye alikuwa ameanguka miongoni mwa wale waliouliwa wakadhani kuwa amekufa akasalimika. Ikamfikia habari ya kuuliwa hawa Masahaba na wale waliouliwa nyuma huko Ar-Raji'i takriban wakati mmoja, na hili likamhuzunisha sana Mtume (SAW) hata akawa anasoma Qunuti mwezi mzima na kuwaombea makabila yaliyofanya uadui huu yaangamizwe, mpaka alipoteremshiwa Wahyi na kusitishwa

Shambulizi dhidi ya Banun-Nadhiir:

            Mauaji haya yaliyotokea dhidi ya Waislamu, yaliwafanya Mayahudi wa Madina kupata moyo kuwa pengine na sisi tunaweza kuwadhuru Waislamu na kurudisha haiba yetu tuliyokuwa nayo zamani, na juu ya kuwa Mayahudi kikawaida si watu wa vita, na ni watu wenye kupenda sana maisha kufikia hadi kuogopa kupigana na kufa, lakini wanajulikana kuwa ni watu wenye njama na vitimbi vingi sana, na daima wanaishi katika hali ya kupanga na kupangua ili kuwatia wenziwao katika taabu na dhiki na shida, ili wao waishi maisha mazuri.

            Kwa hivyo, baada ya mauaji ya Ar-Raji'i na Bir Mauna, Mayahudi walizidi vitimbi na uadui, na safari moja alipokuwa Mtume (SAW) na Masahaba zake wanapita katika mitaa yao, walipanga njama wamuangushie Mtume (SAW) jiwe kubwa kutoka juu ya nyumba ili wamuue, lakini Mwenyezi Mungu alimletea Jibril (AS) na kumpasha habari, akaepuka njama yao hii, na kutoka salama na walipomuuliza Masahaba aliwaeleza njama waliyoipanga Mayahudi ya kutaka kumuua.

            Basi Mtume (SAW) akamtuma Muhammad bin Maslama kwenda kuwaamrisha Mayahudi watoke Madina kwa kuvunja ahadi baina yao na Waislamu na kwa uadui dhahiri waliotaka kumfanyia Mtume (SAW), na akawapa muhula wa siku kumi, baada ya hapo asionekane Yahudi yeyote wa Banun-Nadhiir ndani ya Madina. Mayahudi wakajitayarisha kuondoka, lakini Abdullahi bin Ubay, mkubwa wa Wanafiki, akawaambia kuwa hawana haja kuondoka, na yeye pamoja na Mayahudi wengine na kabila nyengine za kiarabu wenye urafiki nao, wako pamoja na wao. Basi wakapata nguvu na kubaki Madina, na kupeleka ujumbe kwa Mtume (SAW) kuwa wao hawatoki nchi.

            Mtume (SAW) alipopata ujumbe huu alileta takbira na Masahaba wakaleta pamoja na yeye takbira, na kujitayarisha kwenda kupambana na Banun-Nadhiir. Akamweka Ibn Umm Maktum kama mwakilishi wake hapo Madina na kumpa bendera Ali bin Abi Talib, na kuondoka na jeshi kwenda kwa Banun-Nadhiir na kuzizunguka ngome zao.

            Mayahudi kama desturi yao, wakakimbizana na kujificha ndani ya ngome zao, na wakabaki humo masiku fulani wakirusha mishale kutoka juu ya ngome zao, wakitarajia kuwa wenziwao wengine katika Wanafiki na Mayahudi watawasaidia, lakini hapana mmoja aliyetaharaki kufanya jambo, na kwa hivyo, walipoona hata mabustani yao waliyokuwa wakiyategemea kwa chakula yamechomwa moto iliwaingia khofu kubwa, wakamuomba Mtume (SAW) awaruhusu waondoke Madina, na Mtume (SAW) akawaruhusu waondoke wao na wake zao na watoto wao, na kila ambacho ngamia wao wataweza kuchukuwa isipokuwa silaha.

            Basi wakatoka Mayahudi Madina huku wakichukuwa kila ambacho wanahisi wanaweza kuchukuwa, na wasivyoweza kuchukuwa walikuwa wakiviharibu na kuvivunja ili Waislamu wasivipate, wakaondoka na kuelekea Khaybar na wengine wakenda Sham, na wawili tu katika wao ndio waliosilimu na kubakia pale pale Madina, nao ni Yaamin bin Umeyr na Abu Saad bin Wahb

            Mtume (SAW) akapata mali nyingi sana katika shambulizi hili, kwani nyumba zao na ardhi zao na mali zao zilizobakia zote zilikuwa ni za Mtume (SAW), na alipata silaha nyingi sana ngao na panga na silaha nyenginezo. Kisha Mtume (SAW) akawagawia Muhajirina wa mwanzo sehemu na katika Maansari aliwapa Abu Dujana na Sahl bin Hanif kwa umaskini wao, na mali yaliyobaki alikuwa akiwagawanyizia wake zake kila mmoja matumizi ya mwaka na kilichobakia akikitumia kununua silaha kwa ajili ya Jihadi.

Shambulizi dhidi ya Najd: 

            Kwa kutoka nchi Banun-Nadhiir, Waislamu wakazidi kujizatiti na kujimakinisha katika mji wa Madina, kwani wale waliokuwa wakitia chokochoko katika Mayahudi wameondoka aghlabu yao na limebakia kabila moja tu la Banu Quraydha, na Wanafiki wamekashifika na wamekuwa hawana lao jambo, na kwa hivyo, ikabakia kwa Mtume (SAW) kufikiria kuwatia adabu yale makabila ya kibedui yaliyokuwa yakiwakamata Waislamu njiani na kuwaua kwa dhulma na kwa jeuri, ili wafahamu kuwa Waislamu hawakulala na wako tayari kuwarudi wakati wowote ule.

            Basi alipopata habari kuwa makabila ya Banu Muharib na Banu Thaalaba yanajikusanya, hakuwangojea bali alifanya haraka kuwaendea wao na jeshi lake la watu mia saba, na kumweka Uthman bin Affan mwakilishi wake hapo Madina, na kuwaendea walipo huko Najd, na makabila yaliposikia yaliingiwa na khofu kubwa na kukimbilia majabalini, na ikawa ndio dawa yao maana wakakoma kufanya jeuri, na Mtume (SAW) akarudi Madina na jeshi lake, na Waislamu wakatulia nyoyo zao, hasa ilivyokuwa wamekabiliwa na vita vingine na Makureshi ambavyo miadi yake ilikuwa ishakaribia.

Shambulizi la Badr la Pili:

            Miadi aliyoitoa Abu Sufyan kwa Mtume (SAW) ya kukutana tena Badr kwa mapigano iliwadia, na Mtume (SAW) pamoja na Waislamu ni watu wa miadi hawawezi kufunja miadi, na kwa hivyo ulipotimia mwaka Mtume (SAW) alimweka Abdullahi bin Rawaaha mwakilishi wake hapo Madina, na kumpa bendera Ali bin Abi Talib, na kutoka na jeshi la watu elfu moja na mia tano, na kuelekea Badr.

            Huku Abu Sufyan aliondoka Makka na jeshi la watu elfu mbili, lakini njiani ikamuingia khofu kwa kukumbuka yale yaliyowapata katika vita vya mwaka jana, basi alipofika mahali paitwapo Majanna, aliingiwa na uzito mkubwa wa kuendelea na safari na akatumia hila kutaka kuwarudisha wenziwake Makka, akawaambia mwaka huu si mzuri maana kuna ukame na wanyama wetu hawana malisho wala sisi hatuna maziwa ya kunywa, basi bora turudini. Jeshi la Abu Sufyan likavunjika moyo na kuona bora warudi, basi wakafunga safari na kurudi.

            Mtume (SAW) alipowasili na jeshi lake Badr hakuliona jeshi la Abu Sufyan, basi wakabakia hapo siku nane wakiuza na kununua kwenye soko lililokuwa hapo wakapata faida kubwa na kurudi zao Madina bila kupata udhia wowote, na ikawa lawama ni juu ya Abu Sufyan ambaye amehalifu ahadi yake, akalaumiwa sana na Safwaan bin Umayya kwa kitendo hichi. Tukio hili liliwapa Waislamu sifa na haiba kubwa mbele za makabila wengine

Mambo muhimu yaliyotokea mwaka huu:

            Mwaka huu vile vile Fatma binti wa Mtume (SAW) alimzaa mtoto wake Alhusein bin Ali, na akafariki dunia Zaynab bint Khuzayma mke wa Mtume (SAW), na mtoto wa shangazi lake Mtume (SAW) Abu Salama, ambaye mkewe Umm Salama halafu baada ya kutoka eda akaja kuolewa na Mtume (SAW).

Rudi Juu

Matukio ya Tarehe ya Kiislamu kwa Ufupi

Mwaka wa Kikristo Mwaka wa Kiislamu

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
570 K.I 53 B.H. Makka ilihujumiwa na Abraha, akiwa na jeshi kubwa pamoja na tembo (ndovu) ili kuja kuibomoa Kaaba hapo Makka, lakini Mwenyezi Mungu alimuangamiza kwa kumletea ndege waliobeba vijiwe kutoka Motoni.

Abdullah, baba yake Mtume Muhammad (SAW) alifariki dunia.

Mtume Muhammad (SAW) alizaliwa hapo Makkah  katika mwezi wa Rabi-al-Awwal tarehe 12, siku ya Jumatatu.

  51 B.H. Kuzaliwa kwa Abu Bakr Assiddiq (RA)
  48 B.H. Kufariki kwa Amina bint Wahb, mamake Mtume (SAW)
  47 B.H. Kuzaliwa kwa Uthman bin Affan (R.A.)
  46 B.H. Kufa kwa Abdul Muttalib, babu wa Mtume (SAW)
  41 B.H. Mtume Muhammad alichukuliwa safari na ami yake Abu Talib kwenda Syria.

Kuzaliwa kwa Omar bin al-Khattab (R.A.)

591 K.I.   Kisra II aliteuliwa kuwa mfalme wa Masassani
595 K.I. 28 B.H. Mtume Muhammad (SAW) alimuoa Khadijah (RA), mwanamke mtukufu wa Kikureshi, na mfanyi biashara mkubwa.
  20 B.H. Kuzaliwa kwa Ali bin Abi Talib (R.A.)
610 K.I. 14 B.H. Herakle alitawala Kostantinia (Uturuki leo)

Mtume Muhammad (SAW) aliletewa Jibril (AS) kwa mara ya kwanza kumteremshia Wahyi na kumfundisha Qurani. (Q. 96:1-5)

Khadijah na Ali na Abubakar walikuwa watu wa kwanza kuukubali Uislamu.

  9  B.H. Waislamu walihamia Uhabushia (Ethiopia leo)
  8  B.H. Hamza (R.A.), ami yake Mtume (SAW) aliukubali Uislamu, na kadhalika Omar (R.A.) aliingia katika dini ya Uislamu.
  7  B.H. Kabila la Bani Hashim linapigwa pande na Quraish na kutengwa katika Shuab Ali.
  4  B.H. Mwisho wa kupigwa pande Banu Hashim
Kufariki kwa Abu Talib, na Khadijah, mke wa Mtume (SAW).
  3  B.H. Mtume (SAW) anazuru Taif
Kundi la mwanzo la watu wa Madina waliukubali Uislamu
  2  B.H. Mkataba wa kwanza wa Aqaba.
Mtume (SAW) alipelekwa safari ya Israa and Miraji. Israa kutoka Makka mpaka Jerusalemu, na Miraji kutoka Jerusalemu kwenda mbinguni kupokea amri ya Sala na kuonyeshwa mambo ya huko.
  1  B.H. Mkataba wa pili wa Aqaba.
614 K.I.   Jerusalem ilitekwa na Masassani
622 K.I. 1 A.H. Mtume Muhammad (SAW) na wafuasi wake walihamia Madina.

Mwanzo wa mwaka wa kiislamu na kuanza kwa tarehe ya kiislamu, tangu kuhama Mtume (SAW) kwenda Madina katika 1.1.01 A.H., siku ya Ijumaa katika mwezi wa Julai 16, 622 C.E.

Mtume Muhammad (SAW) aliweka msingi wa msikiti wa Quba.  Aidha, msikiti wa Mtume wa Madina ulianza kujengwa.

Waislamu walipewa amri ya kuadhini, na Bilal (R.A.) alikuwa muadhini wa kwanza wa Mtume (SAW).

  2 A.H. Qibla kilibadilishwa badala ya Waislamu kuelekea msikiti wa Al Aqsa waliamrishwa waelekee msikiti mtukufu wa Makka

Waislamu waliamrishwa kufunga mwezi wa Ramadhani.

Vita vya Badr vilipiganwa katika mwezi wa Ramadhani tarehe 17 ya Ramadhan ya mwaka wa pili 2 wa Hijra

Fatima (R.A.) aliolewa na Ali (R.A.)

  3 A.H. Vita vya Uhud
  5 A.H. Vita vya Khandaq
Mtume Muhammad (SAW) alimuoa Zainab bint Jahsh, mtalaka wa Zayd, huru wake na mtoto wake wa kulea.
  6 A.H. Mkataba wa amani wa Hudaybiya
Khalid bin Walid na Amr bin al-Aas waliingia kwenye Uislamu, baada ya mkataba.
Mfalme Najashi wa Habasha (Ethiopia) aliingia kwenye Uislamu.
Mfalme wa Maqipti alimpelekea Mtume (SAW) Maria na nduguye Sirin kama zawadi kutoka kwake. Maria aliingia kwenye Uislamu na Mtume (SAW) akamfanya kuwa suriya wake.
Badhan, mkubwa wa Kifursi hukoYemen, aliingia kwenye Uislamu.
  7 A.H. Vita vya Khaybar vilipiganwa.
Mtume (SAW) alifanya Umrah pamoja na Masahaba zake
Mtume (SAW) alimuoa Safiya, mwanamke wa Kiyahudi baada ya kulishinda kabila lake katika vita, na yeye kuukubali Uislamu.
  8 A.H. Makkah ilitekwa,  na Mtume (SAW) aliingia Makka kama mshindi na kusimama kwenye Al Kabah siku ya Ijumaa tarehe 20 ya mwezi wa Ramadhani na kuamrisha kuvunjwa kwa masanamu.
  9 A.H. Vita vya Tabuk
Mtume (SAW) alipeleka Masahaba zake kwenda kuhiji, wakiongozwa na Abu bakr (RA).
Wasiokuwa Waislamu walikatazwa kuingia kwenye msikiti mtukufu wa Makka kuanzia tarehe hii.
  10 A.H. Hija ya mwisho ya Mtume (SAW) ya kuagaa aliyoifanya pamoja na Waislamu 100,000 na kutoa hotuba yake mashuhuri hapo.
632 K.I. 11 A.H. Mtume Muhammad (SAW) alifariki dunia katika mji wa Madina siku ya Jumatatu, tarehe12 ya mwezi wa Rabi-al-Awwal, akiwa na umri wa miaka 63.
Abu Bakr alichaguliwa kuwa ndiye Khalifa wake wa kwanza.

Hamza na Umar wasilimu

Kuitangaza dini kweupe

Kufikisha Ujumbe kisiri

Bishara ya Utume

Safari ya Sham

Nasaba ya Mtume

Zama za Ujahili Bara Arabu

Shambulizi la Uhud Banu Qaynuqaa Kupanga Udugu Mapatano ya Aqaba Israa na Miraji Majini wanapokea Ujumbe

Mkataba wa dhulma

Waislamu waingia Makka Kutangaa kwa Uislamu Shambulizi la Khaybar Kushindwa kwa Ahzaab Mwaka wa Tano Mwaka wa Nne Abu Sufyan ajinaki
Ukurasa 6 Muhtasari Siku za Mtume za mwisho Mtume (SAW) apokea tume Abubakar (RA) ahiji Kikosi cha A'lqama Washirikina watiwa mbioni