DINI |
UISLAMU
|
![]() |
|||
Maskani | Qurani | Sunna | Fiqhi | Sera | Tarehe | Dua | Masuala | Fatawa | Dunia |
Uislamu | Akhlaq | Nasiha | Mawaidha | Uislamu | Dini | Hidaya | Sikiliza | Uislamu | Viungo |
Tofauti baina ya Uislamu na mila zote nyenginezo ni kuwa dini hii aliteremshiwa baba yetu Adam (AS) pale alipoletwa duniani ili iwe ndio nidhamu yake ya maisha pamoja na kizazi chake mpaka siku ya kiyama, na Mwenyezi Mungu alimwekea mpango huu wa maisha ili aweze kuishi kwa salama na amani hapa duniani kulingana na maelekezo yake na apate radhi zake na Pepo yake kesho Akhera. Kwa hivyo, kinyume na vile watu wengi wanavyofikiri, Uislamu si dini aliyokuja nayo Mtume Muhammad (SAW) peke yake, bali ni dini aliyoletewa binadamu tangu mwanzo alipoteremshwa duniani wakati wa Adam (AS) na kupitia Mitume na Manabii wote wengine waliokuja baada yake mpaka alipoletwa Mtume wa mwisho Muhammad (SAW). Uislamu ulikuja na mambo mawili muhimu: Imani na Sharia. Imani inahusu itikadi yake mwanadamu kuhusu Mola wake, na Sharia inahusu maisha yake hapa duniani katika mambo ya ibada na maingiliano yake na wenzake. Itikadi au Imani kuhusu Mwenyezi Mungu haibadiliki ni ile ile tangu alipoletwa Adam (AS) na kuelezwa kuwa Mola wako ni Mmoja na hana mshirika. Ama Sharia hubadilika kulingana na watu na zama mbali mbali, na kwa hivyo Sharia ya Nuhu inatafautiana na Sharia ya Ibrahim au ya Musa au ya Isa au ya Muhammad, na yote ni kulingana na zama zao na hali za maisha yao. Uislamu aliokuja nao Mtume Muhammad (SAW) ni ujumbe wa mwisho walioletewa binadamu, nao ni ujumbe mkamilifu uliokusanya kila analohitajia mwanadamu katika maisha yake. Ujumbe huu umegusia kila kitu katika nidhamu ya maisha ya binadamu yakiwa ya kijamii au kiuchumi au kisiasa au mengineyo yoyote yale. Ujumbe huu umekuja kunadhimu maisha ya binadamu ili aishi uzuri na kwa wema hapa duniani na akifaulu kufuata nidhamu hii apate radhi za Mola wake na Pepo iwe ndio jazaa yake. Lakini akenda kinyume na nidhamu hii na kufuata matamanio ya nafsi yake, basi atakuwa katika hasara hapa duniani na kesho Akhera atapata adhabu kali kwenye Moto wa Jehanamu. Tume zilizotangulia: Kama tulivyoeleza, Uislamu haukuanza na Mtume Muhammad (SAW), lakini ni dini iliyoletwa na Mitume na Manabii wote wa nyuma tangu Adam (AS), na kwa hivyo tume zote zilizotangulia zinatokana na Mwenyezi Mungu kwa umma mbali mbali, kila umma kwa mahitajio yake, na tofauti ya tume hizi na ujumbe wa Mtume Muhammad (SAW) ni kuwa tume zilizopita ni kwa watu na kaumu fulani na ujumbe wa Mtume Muhammad ni kwa watu wote ulimwenguni. Nchi za kiislamu
|
|