SERA |
MAISHA YA MTUME (SAW)
|
![]() |
|||
Maskani | Qurani | Sunna | Fiqhi | Sira | Tarehe | Dua | Masuala | Fatawa | Dunia |
Library | Biography | Muhammad | Raheeq | Message | Timeline | Brief | Biography | Proofs | Viungo |
Maisha ya Mtume Muhammad (SAW)
Baada ya Mwenyezi Mungu kuleta duniani Mitume na Manabii 123,999 kwa ajili ya kuwaongoza na kuwaelekeza njia ya sawa kaumu zao na watu wao mbali mbali, alimleta Mtume Muhammad (SAW) kuwa ndiye mwenye kukamilisha mfululizo huu wa wajumbe wa Mwenyezi Mungu kwa wanadamu, na akamfanya yeye kuwa ndiye wa mwisho na wa ulimwengu mzima na kwa wanadamu na majini wote. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Muumba wa viumbe vyote alimjaaliya Mtume Muhammad (SAW) kuwa ni kiumbe bora kabisa kuliko wote na kumpa kila sifa njema ambayo mwanadamu mkamilifu anatakiwa awe nayo ili aje kuwa ni mfano na kiigizo kwa wanadamu wengine duniani, na kwa ajili hii, Mtume (SAW) aliishi ulimwenguni akituonyesha mifano mbali mbali katika maisha na namna gani kuishi maisha kikamilifu kwa mujibu wa maelekezo na mafunzo ya mwenyewe Mola aliyetukuka. Mtume Muhammad (SAW) baada ya kwisha kupewa utume alifundishwa kila lenye kheri na binadamu ili awafunze na kuwahimiza na kunabihishwa kila lenye shari na binadamu awazindue na kuwataka wajiepusha nalo ili maisha yao hapa duniani yawe ni mazuri, ya amani na furaha. Akawa yeye ndiye mwenye kuwaonyesha watu mifano hiyo, ili na wao wapate kuigiza na kuifuata. Mtume, kwa hivyo, akaishi kama yatima, mtoto maskini mwenye kufanya kazi utotoni mwake, mvulana na barobaro mwenye kujua na kupigania haki, kijana mwenye kutafuta riziki yake ya halali kwa kufanya biashara kwa uaminifu na juhudi kubwa, mtu mzima mwenye kuaminiwa na watu wake kwa ukweli na uaminifu wake mpaka alipoteuliwa na Mwenyezi Mungu kuwa ni mjumbe wake na kuanza maisha mapya chini ya uwongozi na himaya ya Mola wake. Baada ya kufikiwa na ujumbe kutoka kwa Mola wake na kuchaguliwa kuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa watu wake na kwa umma wa kiislamu kwa jumla, maisha yake yaligeuka na kuwa ni mfano mzuri kwa wanadamu wote kwa jumla. Akawa ni kiongozi mwema na muadilifu, imamu wa waumini katika kumuabudu Mola wao, mwalimu mzuri wa kufundisha kila jema na kukataza kila ovu, mume mwema kwa wakeze na baba mzuri kwa wanawe na rahimu kwa watoto kwa jumla, jirani mwema kwa aliyekuwa Muislamu na asiyekuwa Muislamu, mtu karimu kwa maskini na mafakiri, sahibu mwema kwa wenzake na marafikize, kiongozi mzuri katika hali ya vita na hali ya amani Nchi za kiislamu
|
|