HISTORIA |
TAREHE
|
![]() |
|||
Maskani | Qurani | Sunna | Fiqhi | Sera | Tarehe | Dua | Masuala | Fatawa | Dunia |
Uislamu | Manabii | Mtume | Makhalifa | Umayya | Banu Abbas | Vijidola | Fatimiya | Mauthmani | Viungo |
Historia ya ulimwengu inaanza tangu kuumbwa huu ulimwengu, lakini kwa kuwa kwa muda wa karne nyingi sana binadamu alikuwa ni kitu kisichojulikana ulimwenguni, tarehe ya dunia ilikuwa haijasajiliwa na kwa hivyo ilikuwa haijulikani sawa sawa. Pamoja na hayo, vitabu vyote vya Mwenyezi Mungu vinaeleza kuja kwa mwanadamu duniani na kuchaguliwa kwake kuwa ni mwakilishi na msimamizi wa mambo yake Mola hapa ardhini, na kuwa cheo hiki na jukumu hili amepewa Adam (AS) baba wa binadamu wote, na jinsi ya kizazi chake chote, na kwa hivyo kila mmoja wetu ulimwenguni ni mwakilishi au khalifa wa Mwenyezi Mungu juu ya hii ardhi. Historia ya ulimwengu kwa mujibu wa Kitabu cha mwisho cha Mwenyezi Mungu (Qurani) imegawanyika vipindi vinne: Tangu kuletwa Nabii Adam (AS) hapa ulimwenguni mpaka alipokuja Nabii Nuh (AS), na tangu wakati wake Nabii Nuh (AS) mpaka zama za Nabii Ibrahim (AS), na tangu wakati wa Nabii Ibrahim (AS) mpaka alipoletwa Nabii Muhammad (SAW), na tangu alipokuja Mtume Muhammad (SAW) mpaka Kiyama kitakaposimama. Zama za Manabii na Mitume (AS): Kwa kusahilisha tarehe hii ya binadamu katika ardhi tutazigawa zama hizi katika vipindi viwili tu, navyo ni tangu alipoteremshwa Nabii Adam (AS) na mkewe Hawwa hapa ulimwenguni mpaka aliporufaishwa na kuchukuliwa mbinguni Nabii Isa (AS), na tangu alipoletwa Mtume Muhammad (SAW) mpaka kitakaposimama Kiyama na kukusanywa wanadamu wote mbele ya Mola wao kwa ajili ya kuhukumiwa. Imepokewa kutoka kwa Mtume Muhammad (SAW) kuwa Mwenyezi Mungu alileta ulimwenguni jumla ya 124,000 Mitume na Manabii, wakiwemo katika hao 113 Mitume na waliobakia ni Manabii. Wajumbe hawa waliteremshiwa Wahyi na kutumwa baadhi yao kwa watu wao na kaumu zao kuwaonya shari itakayowafika ikiwa watamkanusha Mola wao na kumshirikisha, na kuwabashiria wema katika wao ambao watashikamana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake kuwa watapata kheri duniani na Akhera. Qurani Tukufu ambacho ni kitabu cha mwisho cha Mwenyezi Mungu kilikuja kutueleza baadhi ya habari za Mitume na Manabii hawa na namna gani Mwenyezi Mungu aliwaneemesha baadhi ya umma zao na kuangamiza wengineo waliokwenda kinyume na maamrisho ya Mola wao. Qurani ilitaja majina ya Mitume na Manabii ishirini na tano (25) waliokuja kwa kaumu mbali mbali na mwisho wake ulikuwaje, ili kutufahamisha sisi faida ya kumfuata Mola na hasara ya kwenda kinyume naye. Wafuatao ni Mitume na Manabii waliotajwa ndani ya Qurani Tukufu na kaumu zao mbali mbali:
Zama za Nabii Muhammad (SAW): Mtume Muhammad (SAW) alipoletwa ulimwenguni aliishi miaka 63, katika hio 40 alikuwa akiishi maisha yake bila kujua nini Imani wala nini Uislamu, lakini baada ya hapo alikuja malaika Jibrili (AS) na kumletea Wahyi na kumfundisha dini ya Mwenyezi Mungu na kuwa chini ya uwongozi na himaya ya Mola wake, na kwa muda wa miaka 23 aliokuwa akipata Wahyi kutoka kwa Mola wake alikuwa ni mfano mwema na kiigizo kizuri kwa Waislamu na kwa wanadamu wote kwa jumla. Wanadamu wote waliokuja baada ya kuletwa Mtume Muhammad (SAW) duniani wanahesabiwa kuwa ni katika umma wa Muhammad, wakigawanyika baina ya wale waliokubali kumfuata yaani Waislamu, na wale ambao hawajamfuata yaani Makafiri, na wao wamegawanyika mafungu matatu: Watu wa Kitabu (Mayahudi na Manasara (Wakristo)), Washirikina na wale ambao hawaamini kuwepo Mwenyezi Mungu kabisa, lakini yote mafungu haya ni katika umma wa Mtume Muhammad (SAW) kwa kuwa yeye ndiye Mtume wa mwisho kwa wanadamu wote. Nchi za kiislamu
|
|