HUKUMU |
FATAWA
|
![]() |
|||
Maskani | Qurani | Sunna | Fiqhi | Sera | Tarehe | Dua | Masuala | Fatawa | Dunia |
Uislamu | Fatawa | Fatawa | Fatawa | Fatawa | Fatawa | Fatawa | Fatawa | Fatawa | Viungo |
Kitabu 25, Namba 3634 cha Abu Daud:
Hadithi hii inatufahamisha umuhimu wa mtu kutafuta elimu hasa ile ya dini kwani dini ndio yenye kunadhimu maisha ya mtu hapa duniani na kumpatia cheo kikubwa kesho Akhera. Wanazuoni wana vyeo vikubwa mbele ya Mola wao na fadhila nyingi kabisa, na kwa sababu hii kila Muislamu anahimizwa kutafuta elimu popote ilipo ili aishi maisha yake akijua nini anachofanya, na aweze kuwaongoza wengineo awatoe kwenye giza la ujahili na kuwatia kwenye mwangaza wa elimu. Kazi hii ya kuwaongoza wengine ni juu ya wanazuoni na maulamaa ambao Mwenyezi Mungu amewajaaliya kupata fursa ya kutafuta elimu ya dini na kujifunza Sharia yake na kujua lipi la halali na lipi la haramu, na ni juu ya watu hawa kuwaelimisha wenziwao na kuwatoa kwenye ujinga na kuwatia kwenye nuru ili waweze kushindana na kumpinga adui wao mkubwa Iblisi na makundi yake ya Mashetani katika wanadamu na katika majini. Hawa wanazuoni na maulamaa, baada ya kuzama katika bahari ya elimu na maarifa na kujua dini yao sawa sawa, hufikia mwisho daraja ya mufti, mtu ambaye mas-ala mbali mbali ya dini huwa na uwezo kutoa hukumu zake katika mambo tofauti tofauti ya maisha. Mufti hutowa fatawa juu ya mambo yanayohusu dini katika maisha ya Muislamu, na fatawa hizi huwa namna mbili: Kuna fatawa kuhusu hukumu mbali mbali za dini ambazo watu wa kawaida huwa hawazijui, na baada ya kuulizwa mwanachuoni mwenye elimu katika mas-ala haya, hutoa fatawa ambayo hutokana na ujuzi wake juu ya hilo jambo. Fatawa nyengine huwa zinahusu mambo katika maisha ambayo Fiqhi au Sharia ya kiislamu haijagusia, katika mambo mapya yanayozuka katika maisha ya binadamu, kama hukumu zinazohusu benki, bima, kununua hisa za mashirika, na mambo menginewe mapya ya ulimwengu wetu wa leo. Fatawa kama hizi zinahitajia ujuzi wa elimu ya dini na kadhalika elimu ya lile jambo linaloulizwa, maana bila ya kuwa na ujuzi wa yote mawili mtu huweza akatoa fatawa za kimakosa na kuwapoteza wengine. Kwa hivyo, inatakikana wanazuoni wachukuwe hadhari katika mambo kama haya. Aidha, kuna fatawa ambazo zinahitajia kukutana maulamaa na wanazuoni wa ulimwengu wa kiislamu na kukubaliana juu ya hukumu ya jambo fulani katika maisha, na makubaliano haya huwa ni itifaki ya maulamaa na fatwa inayotoka huwa ni ijmaa ya umma na kwa hivyo, huwa ni fatwa madhubuti na hukumu ya sawa ya wanazuoni wote, na ijmaa ni mojawapo ya misingi ya dini ya Uislamu baada ya Qurani na Sunna za Mtume Muhammad (SAW). Nchi za kiislamu
|
|