HADITHI |
SUNNA
|
![]() |
|||
Maskani | Qurani | Sunna | Fiqhi | Sera | Tarehe | Dua | Masuala | Fatawa | Dunia |
Uislamu | Bukhari | Muslim | R.Salihin | Sunna | Abudaud | Qudsi | Muwatta | 500hadiths | Viungo |
Mtume Muhammad (SAW) alikuwa na miaka arubaini alipoanza kuteremshiwa Wahyi (Ufunuo) kutoka kwa Mola wake kwa njia ya Malaika mkubwa na mtukufu kabisa aitwaye Jibrili (AS), na kuanzia wakati huo, Mtume Muhammad (SAW) akaanza kufundishwa nini Imani na nini Uislamu. Wahyi uliendelea kuteremka kwa muda wa miaka ishirini na tatu mpaka alipofariki dunia akiwa na umri wa miaka 63, na katika muda huu Qurani Tukufu ambayo ilikuwa ikiteremshwa kidogo kidogo kwake ilikamilika Huu Wahyi ni Maneno ya Mwenyezi Mungu aliyetukuka aliyokuwa akiwateremshia wanadamu tangu alipoletwa Adam (AS) hapa duniani kuwa ndio Khalifa wa hii ardhi, na Wahyi ni mwongozo na mafunzo kwa wanadamu kuwaelekeza njia ya kuishi kwa wema na amani hapa duniani ili kupata radhi ya Mola wao na kutunukiwa Pepo kesho Akhera, na Wahyi alioteremshiwa Mtume Muhammad (SAW) ulikuwa ni Wahyi wa mwisho kuteremshiwa binadamu duniani kwa ajili ya uwongofu wao na uwongozi wao. Katika muda huu wa miaka ishirini na tatu (23) ambao Mtume Muhammad (SAW) alikuwa akipata Wahyi alikuwa akiishi maisha yake chini ya uwongozi na himaya ya Mwenyezi Mungu, na kwa hivyo maneno na vitendo vyake ambavyo alikuwa akisema au akifanya katika kipindi hiki cha Utume wake baada ya kupata Wahyi kutoka kwa Mola wake viliitwa Sunna yaani mwenendo wa Mtume (SAW). Aidha, kila aliloliona au kulisikia katika muda wa Utume wake akalinyamazia kimya au akawa hakulipinga na akalikubali. Vitabu vya Hadithi:Hadithi za Mtume Muhammad (SAW) zimekusanywa katika vitabu vingi sana na wanazuoni mbali mbali wa Hadithi, na hii ni kwa sababu Hadith au Sunna za Mtume (SAW) ni kifafanuzi na kielezo zaidi cha Qurani ili kueleza zaidi mambo yaliyokuja ndani ya Qurani kwa ufupi katika mambo ya Ibada au ya maisha. Vitabu muhimu kabisa vilivyokusanya Hadithi za Mtume (SAW) ni Sahihi Bukhari na Sahihi Muslim ambavyo vinahesabiwa na wanachuoni kuwa ndivyo vitabu sahihi zaidi na vya kutegemewa zaidi baada ya Qurani. Kisha vinafuatia vitabu vya Hadithi vya Tirmidhi, Nasa'i, Ibn Majah, na Abu Daud, ambavyo vinaitwa Sunan navyo pamoja na Sahihi Bukhari na Sahihi Muslim ndivyo vitabu sita vya Hadithi vinavyotegemewa ulimwenguni. Aidha, kuna Muwatta cha Imam Malik, na Musnad cha Imam Ahmad bin Hanbal, maimamu wawili waliokuja na madhehebu ya Kimaliki na Kihanbali.
Aina za Hadithi:Mtume Muhammad (SAW) alikuwa hapendelei ziandikwe Hadithi zake wakati mmoja na Qurani ili yasije yakachanganyika maneno yake na yale ya Mwenyezi Mungu, na kwa hivyo Hadithi zilichelewa kuandikwa mpaka baada ya kufariki kwake dunia kwa muda mkubwa kidogo, na kwa sababu hii Hadithi zikawanyika sehemu mbali mbali kulingana na usahihi wake au udhaifu wake au uwongo wake. Kuna Hadithi aina nne kulingana na fahamu na kutegemewa kwa msimulizi wa hiyo Hadithi. Hadithi Sahihi, Hadithi Hasan (Nzuri), Hadithi Dhaifu, na Hadithi Maudhu'u (Hadithi ya Uwongo). Vile vile, kuna aina nyingine za Hadithi zilizogawanyika kwa mujibu wa mambo mengine kama kwa mujibu wa wapokezi, au mfululizo wa wasimulizi, au idadi ya wasimulizi katika kila sehemu ya mfululizo, au kwa mujibu wa simulizi yenyewe na msimulizi wake. Hadithi kwa mujibu wa fahamu na kutegemewa kwa msimulizi:
Nchi za kiislamu
|
|