Click to see a full-screen photograph

    SHARIA

 

FIQHI

 

       
       
       
       
Maskani Qurani Sunna Fiqhi Sera Tarehe Dua Masuala Fatawa Dunia
Uislamu F.Sunna Islam Learn Knowledge Fiqhi Guide Audio Downloads Viungo

 

Fiqhi: Hukumu za Sharia:

اضغط هنا لعرض تفسير ابن كثير للآية

At Tawba: 9:122

التوبة122:9 

Wala haiwafalii Waumini kutoka wote. Lakini kwa nini hawatoki katika kila kundi miongoni mwao, pote likajifunze vyema Dini, na kisha lije kuwaonya wenzi wao watakapowarejea, ili wapate kujihadharisha?

                          Uislamu umekuja na mambo matatu muhimu nayo ni Imani, Elimu na Amali (Vitendo). Kila Muislamu ili Uislamu wake ukamilike anatakiwa ayakuze mambo haya matatu ili awe karibu na Mola wake na aweze kufuata maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake.

                           Imani ni kumuamini Mwenyezi Mungu mmoja aliyeumba viumbe vyote na kumjaaliya binadamu kuwa ndiye Khalifa wake hapa ulimwenguni. Kwa kuwa yeye ndiye Khalifa au mwakilishi wa Mwenyezi Mungu hapa duniani, na kuwa anahitajiwa aijenge na kuimarisha hii dunia kwa mujibu wa kawaida na misingi ambayo Mola wake amemuekea, binadamu anahitajia kuikuza imani yake kwa kusoma na kujifunza na kuwa na elimu ya dini yake ambayo ndio nidhamu ya maisha yake hapa ulimwenguni..

                           Kila binadamu akitafuta elimu zaidi na kupanua maarifa yake huzidi kuwa karibu na Mola wake kwa sababu ya kumjua zaidi Muumba wake na madhumuni yake ya kumleta hapa ulimwenguni. Kwa hivyo, binadamu anahimizwa kutafuta elimu na maarifa, jambo ambalo litaikuza imani yake zaidi ya kumuamini na kumpenda Mola wake aliyempa kila aina ya neema na baraka hapa ulimwenguni na kumpa cheo kikubwa cha Ukhalifa.

                           Baada ya mtu kuwa na imani na kuikuza kwa kuzidi kutafuta elimu ya dini yake yenye kupanga uzuri maisha yake, anatakiwa na kuhimizwa kuitumia elimu hii katika kufanya ibada zake kwa uzuri na kufanya maingiliano yake baina yake na wenzake kwa wema na hisani ikiwa katika mas-ala ya ndoa na talaka, biashara na mambo yote yanayohusu uchumi, namna ya kuishi vyema na ukoo, jamaa, jirani na kila aliyekuwa Muislamu na asiyekuwa Muislamu.

                           Mambo haya yote ya Ibada na Muamala (Maingiliano) hunadhimiwa na dini ya Kiislamu na Fiqhi au Sharia ya Kiislamu, na yeyote mwenye kujifunza Fiqhi (Sharia) ya Kiislamu huwa amepata tawfiki ya Mwenyezi Mungu ikiwa atafuata yale aliyojifunza, kwani huwa ameingia katika kundi lililotajwa hapo juu la watu ambao Mwenyezi Mungu amewachagua kujifunza dini yake na kuiendeleza na kuwafunza wenzi wake, na hili ni jambo lenye thawabu kubwa na daraja kubwa mbele ya Mola.

                            Na kwa ufupi Fiqhi au Sharia ya Kiislamu inagusia uhusiano baina ya mtu na Mola wake katika mambo ya Ibada kama Sala na Saumu na Zaka na Hija kwa upande mmoja, na uhusiano wake mtu na wenzake hapa ulimwenguni katika mas-ala ya maisha yakiwa katika mambo yanayohusu jamii, uchumi, siasa au mambo yanayohusu amani na vita na uhusiano baina ya makabila na mataifa.

Nchi za kiislamu

Afghanistan

Albania

Algeria

Azerbaijan

Bahrain

Bangladesh

Benin

Brunei

Burkina Faso

Cameroon

Chad

Comoros

Djibouti

Egypt

Gambia

Guinea

G.-Bissau

Indonesia

Iran

Iraq

Jordan

Kazakhstan

Kuwait

Kyrgyzstan

Lebanon

Libya

Malaysia

Maldives

Mali

Mauritania

Morocco

Niger

Nigeria

 Oman

Pakistan

Palestine

Qatar

Saudi Arabia

Senegal

Sierra Leone

Somalia

Sudan

Syria

Tajikistan

Tunisia

 

Turkey

Turkmenistan

UAE

Uzbekistan

      Western Sahara

Yemen

 

Côte d'Ivoire

Ethiopia